Kuunga mkono afya ya vijana

Mombasa ni mji wenye tamaduni na mandhari ya kustaajabisha. Kama Kijana, kuishi hapa kunaweza kuwa jambo zuri na pia kusababisha changamoto kadhaa.

Shirika la Médecins Sans Frontières (linalo julikana pia kama madaktari wasio na mipaka au MSF) limeshirikiana na idara ya afya kaunti ya Mombasa kutoa huduma zilizoimarishwa kwa ajili ya vijana kama wewe.

Ninaweza pata huduma?

Kama una umri wa kati ya miaka 10-24, unaweza pata huduma za afya bila malipo na zenye usiri na zilizopo kwa ajili ya vijana kama wewe!

Jitokeze na kijana wa rika lako atakusaidia kupata huduma unazohitaji. Huduma bure za ushauri kwa ajili ya afya akili pia zinapatikana.

Naweza pata habari wapi?

Ikiwa unapenda kujadili kuhusu huduma na usaidizi, tafadhali jaza kwa ukamilifu fomu hapa chini and tutawasiliana na wewe mda mchache baadaye.